Tuesday , 24th Feb , 2026

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri amefungua shauri la mapitio juu ya uamuzi wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu

Akiwasilisha taarifa hiyo mahakamani leo Wakili wa Serikali Mkuu Renatus Mkude amesema taarifa hiyo mapitio imeungwa mkono na kiap

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri amefungua shauri la mapitio juu ya uamuzi wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu

Akiwasilisha taarifa hiyo mahakamani leo Wakili wa Serikali Mkuu Renatus Mkude amesema taarifa hiyo mapitio imeungwa mkono na kiapo cha Wakili wa Serikali Cuthbert Mbilinyi na imewasilishwa katika mifumo rasmi ya mahakama ya Tanzania leo Februari 24, 2026 na kupokelew Mahakama ya Rufaa ya Tanzania Dar es Salaam kama shauri la mapitio na kupewa namba 7203216/2026.

Wakili Mkude amesema chimbuko la mapitio hayo ni shauri la jinai 19605/2025(kesi ya uhaini inayomkabili Lissu) Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya Mheshimiwa Jaji Dunstan Ndunguru na wenzake wawili.

Ameeleza kuwa kwa kuwa shauri limepokelewa Mahakama ya rufani na limepewa namba basi liweze kusimama ili kutoa nafasi kwa ajili ya maombi kuweza kusikilizwa na baadae kurudi kwenye shauri kuendelea baada ya uamuzi wa Mahakama ya Rufani.

Msingi wa rufaa hii ni uamuzi wa Mahakama uliotolewa leo na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru kuwa ushahidi wa ziada wa ACP Amini Mahamba ambao jamhuri ilitaka kuuwasilisha mahakamani hajakidhi vigezo vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(CPA) kifungu cha 308.

Baada ya hapa Jamhuri iliiomba mahakama kwa kuwa tayari kuna shauri Mahakama ya rufaa basi shauri lililopo mahakama kuu lisimame(kama ambavyo sheria inataka) mpaka litakapokamilika shauri la rufaa.Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri amefungua shauri la mapitio juu ya uamuzi wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu

Akiwasilisha taarifa hiyo mahakamani leo Wakili wa Serikali Mkuu Renatus Mkude amesema taarifa hiyo mapitio imeungwa mkono na kiapo cha Wakili wa Serikali Cuthbert Mbilinyi na imewasilishwa katika mifumo rasmi ya mahakama ya Tanzania leo Februari 24, 2026 na kupokelewa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania Dar es Salaam kama shauri la mapitio na kupewa namba 7203216/2026.