Saturday , 25th Apr , 2026

Baada ya siku kadhaa za sintofahamu, Wekundu wa Msimbazi Simba wameweka nukta!

Klabu ya Simba imethibitisha kuwa mechi ya mzunguuko wa pili ya Ligi Kuu bara ya 'Kariakoo Dabi' dhidi ya Yanga itapigwa katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo, Mei 03.

Simba, ambao watakuwa wenyeji wa mechi hiyo imeamua kuendelea kutumia uwanja huo ambao umekuwa ngome yao kwa sasa, huku mashabiki wakisubiri kuona kama Isamuhyo itatoa mbabe baada ya suluhu ya 0-0 kule Zanzibar (New Amaan Complex) kwenye mzunguko wa kwanza.