Friday , 12th Jun , 2026

Mjasiriamali Zari The Bosslady ameshea nasi taarifa ya kuvunjika kwa ndoa yake na aliyekuwa mumewe Shakib baada ya kudumu kwa miaka mitano.

Zari na Shakib enzi za ndoa yao

Kupitia 'Insta Story' yake akieleza kwamba wamechukua uamuzi huo mgumu baada ya kutafakari na kufikiria sana na wanaamini utakuwa sahihi sababu ya kutokea tofauti isiyoweza kusuluhishwa.

Zari ameendelea kueleza maamuzi hayo hayakuwa mepesi lakini wanashukuru kwa kila muda waliokuwa pamoja kati yao, vitu walivyoshea pamoja na kumbukumbu safi walizozitengeneza.