Tuesday , 16th Jun , 2026

Dakika 90 dhidi ya Hispania kwenye Kombe la Dunia zimebadilisha maisha ya golikipa wa Cape Verde, Josimar Dias.

Baada ya kuonyesha kiwango cha juu na kuisaidia Cape Verde kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Hispania, mashabiki wa soka duniani walimiminika kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kumpongeza kwa umahiri wake langoni.

Kabla ya mchezo huo, Josimar alikuwa na takribani wafuatiliaji 50,000 kwenye Instagram,lakini ndani ya muda mfupi baada ya mechi, idadi hiyo ililipuka na kufikia zaidi ya milioni 4.7 mpaka sasa kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwa Josimar Dias, mchezo mmoja dhidi ya moja ya timu kubwa duniani umegeuka kuwa tiketi ya kutambulika na dunia nzima, hii ndiyo ile wanasema Mungu akitaka kukupa hakuandikii barua.