Tuesday , 16th Jun , 2026

Marcus Rashford amerudi rasmi kuwa mchezaji wa Manchester United baada ya klabu ya Barcelona kuruhusu kipengele cha kumnunua kwa kudumu cha euro milioni 30 (£26m) kupita bila kukiwasha kabla ya tarehe ya mwisho ya Juni 15, 2026

Marcus Rashford

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alikuwa na msimu mzuri wa mkopo huko Camp Nou, akifunga mabao 14 na kutoa asisti 14 katika mechi 49. 

Hata hivyo, matatizo ya kikomo cha mishahara (financial fair play) na usajili mpya wa Anthony Gordon kutoka Newcastle vimezuia Barcelona kukamilisha dili hilo la kudumu

Uongozi wa Manchester United hautaki kusikia kabisa habari za ofa nyingine ya mkopo. Wanataka kumuuza moja kwa moja ili kuondoa mshahara wake wa pauni 325,000 kwa wik

Kwa sasa, Rashford ameweka kando masuala ya usajili na anaangazia michuano ya Kombe la Dunia la 2026 akiwa na timu ya taifa ya Uingereza huko Marekani, huku wakala wake akiendelea kutafuta suluhu ya kudumu ya mustakabali wake wa klabu