Friday , 19th Jun , 2026

Grammy-nominated producer Tay Keith, ambaye jina lake halisi ni Brytavious Lakeith Chambers, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 29.

Mwili wa Keith ulikutwa ndani ya apartment yake huko Nashville, Tennessee baada ya watu wake wa karibu kushindwa kuwasiliana naye kwa muda na kuomba msaada kwa Polisi.

Kutokana uchunguzi wa awali Polisi wamesema hakuna dalili za uhalifu kwenye tukio hilo na sababu ya kifo chake bado haijafahamika lakini bado wanaendelea kufuatilia kujua chanzo cha kifo chake.

Tay Keith alikuwa mmoja wa producers wakubwa kwenye muziki wa Hip-Hop na Trap nchini Marekani aliyefahamika zaidi kwenye nyimbo kama "Sicko Mode" - Travis Scott wimbo uliofanikiwa kufika kushika namba moja kwenye 'Billboard Hot 100' na kupata Grammy nomination na "Look Alive" ya BlocBoy JB na Drake ambao ulimfanya ajulikane kimataifa mwaka 2018.