.... baada ya Ismaël Koné, kulazimika kutolewa nje ya uwanja kwa machela baada ya kupata jeraha baya linaloonekana kuwa ni kuvunjika mguu.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mapema kipindi cha pili katika uwanja wa BC Place baada ya Koné kufanyiwa madhambi na mchezaji wa Qatar, Assim Madibo, ambaye alionyeshwa kadi nyekundu.
Hata hivyo, dakika 10 tu baada ya Koné kutolewa uwanjani, mchezaji aliyeingia kuchukua nafasi yake, Nathan Saliba, alifunga goli la nne la Canada.
Saliba aligusa mioyo ya mashabiki wengi kwa kusherehekea goli hilo huku akiwa ameinua juu jezi namba 8 ya mchezaji mwenzake huyo aliyeumia.





