Mbunge kutatua tatizo lililodumu zaidi ya miaka 20
Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima, amesema hataki kuwa kama wabunge waliopita ambao walishindwa kutatua changamoto ya mtaro wa kupitisha maji ili kuzuia mafuriko ya mara kwa mara iliyodumu kwa zaidi ya miaka 20 katika eneo la Kunduchi Pwani.