Ronaldo aendelea kuweka rekodi Ureno

Nahodha wa Ureno Criastiano Ronaldo amefunga goli lake la 133 akiwa na jezi ya timu ya Taifa lake kwenye mchezo waliocheza ugenini dhidi ya Poland siku ya jana Oktoba 12, 2024, kumfanya aendelee kuiweka vizuri rekodi yake ya kuwa Mchezaji aliyefunga goli nyingi kwenye michezo rasmi ya kimataifa kwa upande wa Wanaume. Kwenye ushindi dhidi ya Poland Ronaldo amefikisha goli la 903 tangu aanze kucheza soka.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 38, anapambania kufikisha goli 1000 katika maisha yake ya kucheza mpira wa miguu kama atafikisha idadi hiyo atakuwa Mchezaji pekee aliyefunga goli nyingi kuliko yeyote kwenye michezo rasmi ya kimashindo. Bado goli 94 afikishe idadi ya magoli 1000.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS