Mauaji nchini yamnyima usingizi Waziri
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, amesema tangu ateuliwe kuongoza Wizara hiyo yapo mambo mawili yanayomnyima usingizi ikiwemo mauaji yanayotekelezwa na baadhi ya watu kwenye jamii pamoja na baadhi ya askari kufanya vitendo kinyume na maadili.

