Wanafunzi hatarini kuangukiwa ukuta
Wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kododo Tarafa ya Mgeta wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wapo katika hatari ya kuangukiwa na madarasa wanayoyatumia kufuatia madarasa hayo ambayo yamejengwa kwa mawe tangu mwaka 1970 kuanza kupasuka kisha kudondosha mawe.