Kariakoo kufungwa CCTV Camera
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, amesema kuwa bajeti ya Jiji itakayopitishwa kwa mwezi Desemba, watahakikisha wanapambana kuingiza bajeti ya kununua CCTV camera na taa zitakazofungwa katika soko la Kariakoo ili liwe eneo salama zaidi kwa wafanyabiashara.