Mauaji nchini kujadiliwa Dodoma
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amewaita watendaji wakuu wa Jeshi la Polisi, ofisini kwake Dodoma, siku ya Jumatatu ya Januari 31, 2022, ili kupokea taarifa na kujadili jinsi ya kudhibiti matukio ya mauaji ya kijamii yanayotokea nchini.

