CHADEMA kurudishiwa mamilioni yao ya faini
Mahakama Kuu imetengua hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, iliyowatia hatiani Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake nane, waliohukumiwa kifungo ama kulipa faini ya shilingi milioni 350 ambapo Mahakama hiyo imeelekeza faini zilizolipwa zirudishwe kwa wahusika.

