Mbunge apongezwa kwa kutopiga sarakasi Bungeni
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh. Godfrey Kasekenya, amempongeza Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay, kwa kutopiga sarakasi Bungeni, baada ya serikali kutangaza kuanza ujenzi wa barabara inayotoka Mbulu, Haidom hadi Singida kwa kiwango cha lami.

