Miili ya watu 5 waliokufa maji Singida yapatikana
Miili ya watu watano akiwemo mwanafunzi wa kidato cha nne waliokuwa wakihofiwa kufa maji Wilayani Singida imepatikana na kuopolewa baada ya juhudi za askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka mikoa mitano kushirikiana na wavuvi eneo hilo.

