Michango ya kwenye shule ni hiari- Silinde
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhe. David Silinde, amesema michango inayoruhusiwa katika suala la elimu ni uchangiaji wa hiari na hauhusishi wanafunzi kuzuiwa kuhudhuria masomo.