James Harden awatega pabaya Brooklyn Nets NBA
Mlinzi nyota na tegemezi wa timu ya Brooklyn Nets, James Harden huenda akaukosa mchezo wa mzunguko wa pili wa Nusu fainali ya NBA kwa ukanda wa Mashariki baada ya mkali huyo kupata maumivu makali ya misuli hadi kushindwa kuendelea na mchezo dhidi ya Milwaukee Bucks.