Mama aibiwa mtoto hospitali, aeleza mazingira
Mtoto David Mfambo mwenye umri wa siku saba ameibiwa katika hospitali ya wilaya ya Frelimo mkoani Iringa, baada ya Mama mzazi kurubuniwa na mwanamke asiyemjua aliyemdanganya kwamba amshikie mtoto wake na kisha yeye kumuagiza akamchukulie kitu nje na aliporudi hakumkuta.