Mbunge ahoji Darasa la 7 kukosa ajira serikalini
Mbunge wa Viti Maalum Nusrat Hanje, amehoji ni kwanini vijana waliomaliza darasa la saba hawapewi fursa ya kuajiriwa na taasisi za serikali hata kama wanazo fani walizozipata kupitia vyuo vya ufundi vinavyotambulika na serikali kwa kigezo cha kutokuwa na cheti cha kidato cha nne.