Rais aeleza maneno ya mwisho aliyoongea na Mfugale
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa mara ya mwisho kuonana na aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale ni mkoani Mwanza kwenye daraja la JPM ambapo alimpa maelezo ya kina jinsi atakavyolijenga na kulikamilisha daraja hilo la Kigogo- Busisi.

