Ukosefu wa Ajira wazidi kuongezeka Uingereza
Ukosefu wa ajira nchini Uingereza umefikia asilimia 5.2, kiwango ambacho hakijashuhudiwa kwa zaidi ya miaka mitano, huku kasi ya ongezeko la mishahara ikishuka hadi asilimia 4.2, kulingana na takwimu zilizotolewa na Office for National Statistics (ONS).

