Tamko la wizara kwa vijiji vilivyovamiwa na tembo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Mary Masanja amesema kuhusu suala la fidia kwa vijiji vilivyovamiwa na tembo wamekuwa na utaratibu wa kufanya uthamini pale changamoto hiyo inapotokea na kisha hulipa fidia wananchi kulingana na athari ilivyojitokeza.