Juventus yaweka wazi hatma ya Ronaldo
Makamu wa rais wa klabu ya Juventus ya Italia, Pavel Nedved amesema hawana mpango wa kuachana na nyota wake Cristiano Ronaldo msimu huu na wanataraji nyota huyo ataendelea kuwepo klabuni hapo kwa mwaka mmoja zaidi hadi kufikia mwisho wa mkataba wake mwaka 2022.