Hii ndiyo idadi ya waliotazama kuagwa kwa Magufuli
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa karibu ya watu bilioni 4 duniani kote, wametazama kupitia vyombo vya habari zoezi la kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, ambalo kitaifa lilifanyika jana Jijini Dodoma.