Hatma ya Chelsea na Atletico Madrid kujulikana leo
Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inataraji kuendelea tena saa 5:00 usiku wa leo kwa michezo miwili ya mkondo wa pili hatua ya 16 bora, mabingwa watetezi, Bayern Munich watawakaribisha Lazio huku wakiwa na faida ya mabao 4-1 ilhali Atletico Madrid watachuana na Chelsea wenye faida ya bao 1-0.