Curry na rekodi ya kipekee Golden State Warriors
Mchezaji nyota wa Golden State Warriors, Stephen Curry ameweka rekodi ya kuwa mcheza kikapu namba moja kwa kutengeneza mabao kwenye klabu yake hiyo baada ya alfajiri ya kuamkia leo kutengeneza mabao mengine mawili wakati timu yake ilipofungwa na LA Lakers kwa alama 128-97.