Guardiola asema haya baada ya kufuzu robo UEFA
Kocha wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa wapo makini sana baada ya timu yake kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya usiku wa kuamkia leo kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani.