Waziri Mhagama atoa wiki mbili mradi ukamilike
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, ameiagiza kamati elekezi ya kusimamia mradi wa Mkulazi Estate, kuhakikisha ndani ya wiki mbili ujenzi wa barabara na uwekaji umeme kwenye eneo la mradi unakamilika.