Shule zakutwa na mabweni kama magofu
Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu, kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera, wamezifungia shule mbili za msingi ambazo ni Kido na Talent kutoa huduma ya bweni, kutokana na majengo yanayotumika kuwalaza wanafunzi kuwa na hali mbaya isiyofaa kutoa huduma hiyo.