Konyagi yabadili nembo ili kuwatambua wanawake

Mtaalamu wa masuala kidigitali (Digital Specialist) Bi Lilian Flavian (Katikati) akipokea zawadi ya kinywaji cha Konyagi yenye muonekano wa nembo ya mwanamke badala ya nembo iliyoezoeleka ya mwanaume shupavu ikiwa ni ishara ya kutambua weledi, ujasiri na taaluma za Wanawake walio na mchango chanya kwenye jamii. Chupa hizo maalum zina nembo yenye mwanamke aliyenyanyua mikono juu na ujumbe wa kuwatakia waTanzania heri ya siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka. Wanaomkabidhi zawadi ni wawakilishi kutoka kampuni ya Tanzania Distilleries Limited watengenezaji wa kinywaji hicho.

Katika jitihada za kutambua weledi, ujasiri na taaluma za Wanawake walio na mchango chanya kwenye jamii, kampuni ya Tanzania Distilleries Limited  kupitia kinywaji chake cha Konyagi imebadili muonekano wa nembo ya kinywaji hicho ikiwa na picha ya mwanamke katika nembo yake iliyozoeleka

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS