Diaspora wenye fedha kufuatiliwa
Serikali imesema kuwa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, itahakikisha inawafuatilia Watanzania wenye fedha wanaoishi nje ya nchi ili waweze kuja kuwekeza hapa nchini kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.