Polisi watoa neno ajali iliyouwa wanne
Watu wanne wamefariki dunia, akiwamo Afisa Ugavi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) mkoa wa Simiyu, Castory Mamboleo (35), kufuatia ajali iliyohusisha magari mawili wilayani Bariadi, mkoani humo.