Waziri aagiza mameneja hawa wabadilishwe
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amemuagiza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Cyprian Luhemeja, kubadili mameneja wote jijini hapo ili kuboresha huduma za usambazaji maji katika maeneo yote yanayosimamiwa na mamlaka hiyo.