Azam kuzigomea Bilioni 2.3 za Raja Casablanca
Uongozi wa Klabu ya Azam umesisitiza kwamba licha ya uwepo wa taarifa zinazoenea mitandaoni kwamba Raja Casablanca ya Morocco imekusudia kulipa kiasi cha Bilioni 2.3 za kitanzania kumsaini mshambuliaji wao Prince Dube, wao hawatomuuza nyota huyo.