Tahadhari ya magonjwa ya mlipuko yatolewa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imetoa tahadhari na kuagiza kuchukuliwa hatua za kuepuka kutokea kwa magonjwa ya mlipuko, kufuatia mvua zinazoendelea katika baadhi ya maeneo na kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu hasa kwa mkoa wa Dar es Salaam.