Meridian Bet, Lions waungana kuinua Sekta ya Afya
Kampuni ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet na klabu ya Lions, zimesaidia kampeni ya upimaji,matibabu na ushauri nasaha ya magonjwa ya macho, sukari na shinikizo la damu, yaliyotolewa bure kwenye hospitali ya Polisi Kilwa road, Jijini Dar es Salaam.