Uamuzi wa Serikali kwa wanafunzi waliopo China
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewatoa hofu na taharuki Watanzania hususan wazazi, ndugu na jamaa wa wanafunzi takribani 420 walioko katika jimbo la Hubei, mji wa Wuhan Nchini China, ambapo ndio kitovu cha maambukizi ya virusi vya homa ya Corona (COVID-19).