Serikali kumsaka aliyejinadi anatibu Corona
Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile, amesema kuwa Serikali imekwishatuma wataalam wake kwa ajili ya kumhoji Nabii namba saba aliyejitokeza na kutangaza kuwa anao uwezo wa kutibu ugonjwa wa homa kali ya mafua inayosababishwa na Virusi vya Corona na iliyopewa jina la COVID-19.