Wizara yaeleza suala la Makonda kuzuiliwa Marekani
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema kuwa hadi leo Februari 2,2020 haijapokea waraka wowote unaotoa taarifa za kumzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwenda nchini Marekani kama ambavyo taarifa zinasambaa mitandaoni.