Magufuli asikitishwa na idadi kubwa ya vifo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ametuma salamu za rambirambi kwa familia za watu 20 waliopoteza maisha jana Februari 1, 2020, wakati wakikimbilia kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la Mtume Boniface Mwamposa, mkoani Kilimanjaro.