Mama Sitta aangua kilio Bungeni
Mke wa aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Samwel Sitta, Bi Margaret Sitta, leo ameangua kilio bungeni wakati akipokea joho alilokuwa akilivaa marehemu mumewe wakati wa kuongoza vikao vya Bunge.