Aliyeiba nguo za ndani 100 akutwa amevaa 2
Mwanaume mmoja mwenye tabia ya Wizi wa nguo za ndani za wanawake, anayejulikana kwa jina la Mukoshi Chipukosia (36), kutoka kijiji cha Hirumbi nchini Kenya, amekamatwa na kufikishwa kwa Mjumbe wa Nyumba Kumi kwa kosa la kuwaibia wanawake nguo za ndani 100 na kukutwa amevaa mbili.