Polisi Tanga wakamata mirungi kutoka Kenya
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limetekeleza operesheni ya mafanikio usiku wa kuamkia leo Julai 22,2025 kwa kukamata boti aina ya fibre, rangi nyeupe, iliyokuwa ikisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kutoka nchini Kenya kupitia Bahari ya Hindi.