Polepole azungumzia 'kumpongeza' Zitto Kabwe
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amekosoa maandamano mbalimbali ambayo yamekuwa yakilenga kuwapongeza baadhi ya viongozi wa nchi kwa kile alichokidai kuwa huenda yakaleta machafuko kwa baadhi ya waandamanaji.