Polisi wajiweka sawa kusherehekea mwaka mpya
Jeshi la polisi Mkoani Iringa limepiga marufuku vitendo vya uchomaji matairi pamoja na ufyatuaji wa fataki katika mkesha wa mwaka mpya na kusema vitendo hivyo vimekua chanzo cha kuongezeka kwa uhalifu wakati wa msimu wa sikukuu.