Simu yatumika kuendesha kesi ya Mbowe na Matiko
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Sam Rumanyika, amelazimika kupiga simu akiwa ndani ya chumba cha Mahakama na kuzungumza karani wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati wa kusikiliza rufaa ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.