Utata waendelea kutawala milioni 50 za Mtibwa
Baada ya hivi karibuni kubainika kuwa klabu ya soka ya Mtibwa Sugar haijalipwa fedha zake za kushinda ubingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho, kiasi cha shilingi milioni 50, pande mbili husika ambazo ni TFF na mdhamini, zimeendelea kutupiana mpira.