Dkt. Mengi kuja na kiwanda cha magari
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi leo ametia saini mkataba wa makubaliano baina ya IPP Automobile Ltd na kampuni ya Youngsan Glonet Corporation ya Korea Kusini kwa ajili ya uanzishaji wa kiwanda cha kuunganisha magari nchini kitakachoanza kazi mwakani.