Aslay amtaka Mzee Yusuph amuombee
Msanii wa bongo fleva ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha 'Subalkheri mpenzi' alichoshirikiana na mwanadada Nandy, Aslay amemuomba Mzee Yusuph amuombee dua ili nae siku itakapofika basi arudi katika dini japo kwa sasa hajatizamia hilo.